News
Loading...

NASRI ALIPANGA NJAMA NIPIGWE SHOTI YA UMEME NIPOOZE NISICHEZE MPIRA TENA!! GALLAS

Beki wa zamani wa klabu ya Arsenal ya England mfaransa William Gallas amefunguka na kuweka wazi kilichokuwa kinapangwa na mfaransa mwenzake Samir Nasri ambaye alikuwa na matatizo nae kwa muda mrefu na hawakuwa wakielewana wala kuongea kwa msimu mzima.
Gallas ameweka wazi kuwa Nasri alifanya njama mwaka 2009 wakiwa Arsenal amuitie watu wampige shoti ili apooze, hiyo ni baada ya Gallas kumkosoa Nasri katika kitabu chake cha historia yake ya maisha mwaka 2008.
nasrigallas
“Nilikuwa na binamu yangu tukila chakula lakini ilikuwa ni usiku ambao tulitakiwa kujiunga timu ya taifa, baada ya kula nilitoka nje ya hotel kuna mtu akaja kuomba kutaka tuongee na aliomba nikakutane na Nasri ambaye alikuwa kwenye gari umbali mchache”
“Nilikuwa tayari kwenda kuonana na Nasri sema binamu yangu ambaye ni polisi alinikataza, lakini baadae niliona katika begi la yule jamaa likiwa na kifaa cha kupigia shoti (taser) kwa bahati nzuri kulikuwa kuna watu eneo lile na sijui kama ningeenda kingetokea nini”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment