News
Loading...

KOCHA WA SIMBA AWAAMBIA VIONGOZI WAKE HATAKI KIKOSI CHAKE KIPANGULIWE!!

Picha inayohusiana

Bosi wa benchi la ufundi la Simba, Joseph Omog, yupo kwao Cameroon kwa mapumziko lakini amewaambia viongozi wa timu yake kwamba hawatakiwi kukipangua kikosi ili kifanye vizuri baadaye.

Omog amewataka mabosi wake kutokitibua bila maelekezo yake kikosi chake kilichocheza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara badala yake wanatakiwa kukiongezea nguvu ili kifanye vizuri zaidi.

Hadi sasa Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 35 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 33 huku timu zote zikiwa zimecheza mechi 15.

Akizungumza kabla ya kuondoka nchini, Omog alisema wakati huu wa usajili wa dirisha dogo, mabosi wake wanatakiwa kuyafanyia kazi mapendekezo yake aliyoyawasilisha kwenye ripoti na wasichukue uamuzi wa kuwatema wachezaji muhimu kikosini.

“Hatutakiwi kukiondoa kikosi hiki cha kwanza kwa namna yoyote ile kwa sababu kimetusaidia kufikia mafaniko haya, hivyo kumpoteza mchezaji yeyote yule aliyecheza katika mzunguko wa kwanza, litakuwa pigo kwa sababu ana umuhimu wake na bado wote nawahitaji katika kufanikisha kutwaa ubingwa.

“Cha muhimu wao wafanye kile ambacho tumekijadili kwenye ripoti kwa kuongeza mshambuliaji pamoja na mabeki wa kushoto na kulia kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi,” alisema Omog.

Tangu Novemba 15, mwaka huu timu za ligi kuu zipo katika usajili wa dirisha dogo ambalo litafungwa Desemba 15 na siku mbili baadaye mzunguko wa pili wa ligi hiyo utaanza
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment