Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya SportPesa yataanza kutimua vumbi Juni 5 kwa Yanga kuwavaa Tusker ya Kenye kwenye Uwanja wa Taifa.
Cannavaro amesema mashindano hayo yamekuja katika wakati mgumu kulingana na changamoto lukuki zinazowakabili.
“Kwa sababu ni mashindano lazima tushindane hivyo wachezaji niwaombe tujitahidi kadri tunavyoweza kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa mara ya kwanza kuweke historia.”
Cannavaro alisema moja ya changamoto kwao kwa sasa ni wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kuwa katika majukumu ya timu za taifa na wengine kumaliza mikataba yao huku baadhi yao wakiwa kwenye mfungo wa ramadhani.
Alisema pamoja na changamoto lukuki, lakini tutahakikisha tunatwaa ubingwa huo kuzima tambo za Simba baada ya kutwaa Kombe la FA.
0 comments :
Post a Comment