Wiki ya 14 ya Premier League ilishuhudia jumla ya magoli 37 yakifungwa na kadi 3 nyekundu kutolewa lakini pia magoli mawili ya kujifunga na hat-trick moja. Tukiwa tunaelekea wiki nyingine ya 15 ya Premier swali ni je nani atafanya nini katika wiki hii wakati chelsea ikijaribu kuchanja mbuga katika uongozi wa ligi hiyo?
Mtandao wako wa Mwanaspotrs leo umefanya tathimini ya michezo ya wiki hii kukupa mwanga wa michezo hiyo.
Burnley vs Bournemouth (Turf Moor, Saturday 15:00)
Team news
Burnley
Team news
Burnley
- Golikipa Tom Heaton atakuwa akirejea katika kikosi cha Burnley mchezo wa kesho dhidi ya Bournemouth.
Heaton alikosekana katika michezo miwili kufuatia maumivu ya kiazi cha mguu lakini amefanya mazoezi vizuri na bila shaka atakuwa akichukua nafasi yake iliyokuwa inashikiliwa na Paul Robinson.
Winga Johann Berg Gudmundsson hatakuwepo kufuatia majeraha ya paja ilhali Steven Defour na Sam Vokes watakuwa wakirejea katika kikosi cha kwanza XI.
Bournemouth
- Bournemouth itakuwa na nguvu mpya ya mlinzi wake kwa kushoto Charlie Daniels itakapo kuwa ikielekea kuwafuata Burnley baada ya kuponya mamumivu ya kiuno.
Junior Stanislas ana uguza nyonga ya mguu ambayo inamuondosha kikosini kwa wiki kadhaa.
Kiungo Andrew Surman, ambaye amekosekana tangu Oktoba anaendelea kuponya maumvu ya nyama za paja.
Takwimu muhimu za mchezo huu
Burnley haijawahi kupoteza mchezo ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Turf Moor dhidi ya Bournemouth katika mashandano yote waliyokutana (W7 D6 L0).
Bournemouth maarufu kama ‘Cherries’ haijashinda katika michezo yao sita ya mwisho ya mashindano mbalimbali dhidi ya Burnley (D3 L3), mara ya mwisho ilishinda 5-0 Novemba 1998 zikikutana kwa mara ya tatu.
Katika utumishi wake wa vipindi viwili vya umeneja wa Bournemouth, Eddie Howe aliwahi pia kuwa meneja wa Burnley, akishinda mara 34 katika michezo 87 ya ligi akiwa na Clarets (39%).
Hii ni mara ya kwanza kwa vikosi hivi kukutana katika ligi ya daraja la juu (Top-flight).
Bournemouth wataingia katika mchezo huu wakijaribu kupata matokeo ya ushindi mfululizo katika Premier League kwa mara ya kwanza tangu mwezi Machi.
Burnley wana uguliwa vichapo vitatu mfululizo vya Premier League wakiwa wameruhusu kufungwa magoli nane katika michezo hiyo mitatu na wao wakifunga goli moja.
Leicester vs Manchester City (King Power Stadium, Saturday – 17:30)
Team news
Leicester (Mbweha)
Team news
Leicester (Mbweha)
- Kipa namba moja wa Leicester Kasper Schmeichel anaweza kurejea kulinda milingoti mitatu katika hali ya kushangaza dhidi ya Manchester City ikiwa ni mapema Zaidi baada ya kuvunjika mkono.
Danny Drinkwater anaendelea kutumikia adhabu ya kusimama mchezo mwingine wa Premier League lakini Jamie Vardy, Riyad Mahrez, Islam Slimani, Robert Huth na Andy King watakuwa kazini baada ya kuachwa katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya ambao walikula kichapo kipana cha bao 5-0 kutoka kwa Porto katikati ya wiki.
Manchester City
- Sergio Aguero, Fernandinho na Nicolas Otamendi wote wanatumikia adhabu za kusimama michezo kadhaa.
Takwimu muhimu za kuelekea mchezo huo
- Manchester City haijapoteza katika uwanja wa ugenini (King Power Stadium) dhidi ya Leicester katika ligi ya Premier (D2 L3), kwani mchezo wa mwisho kufungwa dhidi ya Leicester ulikuwa Machi 1987.
Claudio Ranieri ameshinda michezo saba ya Premier League dhidi ya Manchester City, huku sare pekee ikitokea King Power Stadium msimu uliopita.
Manchester City imeshinda michezo sita dhidi ya bingwa mtetezi lakini wakipoteza dhidi ya Chelsea mwezi Machi 2011.
Chelsea vs West Brom
- Chelsea watakuwa wenyeji wa West Brom katika wiki ya 15 ya Premier League mwisho wa wiki hii wakijaribu kuendeleza mwenendo wao mzuri wa ushindi kwa ushindi wa uwanja wa nyumbani.
Chelsea wako juu ya msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 3 na anayemfuatia.
Huu unaweza kuwa ni ushindi wake wa nane mfululizo.
Wanaingia katika mchezo huu wakiwa na rekodi nzuri dhidi ya West Brom katika misimu ya hivi karibuni jambo ambalo linawapa nguvu ya kufanya vema katika mchezo huo.
Antonio Conte anaweza kukosa huduma ya wachezaji wake nyota Diego Costa na Pedro Eliezer Rodriguez Ledesma. Nemanja Matic huenda naye akakosekana kama ilivyo kwa John Terry ambaye anaendelea kuponya majeraha.
WEST BROM TEAM NEWS & PREVIEW
- West Brom inaelekea katika mchezo huu wakiwa na mfululizo wa ushindi katika michezi mitatu kati ya minne ya hivi karibuni.
Kikosi cha Tony Pulis bila shaka kitakuwa kinataka kutumia mchezo wa kujilinda Zaidi kikiwa ugenini. West Brom kimekuwa kikosi kigumu kufungika hivi karibuni na kwakuwa wachezaji hatari Costa na Pedro watakosekana katika kikosi cha Chelsea hii itakuwa ni nafasi nzuri kwa wageni kushinda katika mpango wao wa ulinzi.
Boaz Myhill na Saido Berahino watakosekana katika kikosi cha wageni.
Takwimu muhimu kwa timu hizi zinapokutana
- Chelsea imeshinda michezo yake 8 ya mwisho ya Premier League.
Chelsea haijapoteza michezo yake 10 ya mwisho dhidi ya West Brom ya mashindano yote.
Chelsea imekuwa na takwimu nzuri za ufungaji kuanzia goli mbili katika michezo 7 kati ya 8 ya Premier League.
Manchester United vs Tottenham
- Tottenham inaelekea Manchester United wikiendi hii kwa lengo la kupunguza pengo kati yao na wapinzani wao.
Kikosi cha meneja Mauricio Pochettino kimepoteza mchezo mmoja tu msimu huu ilhali mashetani wekundu hakijashinda katika ardhi ya Old Trafford tangu kiliposhinda dhidi ya bingwa mtetezi wa taji Leicester mwezi Septemba.
Spurs itakuwa ikiingia katika mchezo huu wakiwa na hali ya kujiamini Zaidi baada ya ushindi mpana dhidi ya CSKA Moscow.
TEAM NEWS
- Toby Alderweireld yuko sawa kiafya ya mchezo baada ya kuingia katika kipindi cha pili mchezo wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya CSKA Moscow.
Spurs imepona kutoka katika ugonjwa wa kushindwa kufunga magoli mengi huku Dele Alli akionekana kama mwiba mbele ya United
Eric Dier atakuwa anarejea katika kiungo cha Spurs licha ya kwamba atakuwa katika ushindani wa kuanza mbele ya Victor Wanyama, Mousa Dembele na Harry Winks.
Eric Dier atakuwa anarejea katika kiungo cha Spurs licha ya kwamba atakuwa katika ushindani wa kuanza mbele ya Victor Wanyama, Mousa Dembele na Harry Winks.
Chris Smalling bado anauguza kidole lakini Luke Shaw ameponya maumivu yake ya mguu.
Michael Carrick, Antonio Valencia na Matteo Darmian wote walisalia nyumbani wakati wa safari ya kuelekea Zorya Luhansk, ikifikiriwa pengine wakatumika katika dhidi ya Spurs.
Eric Bailly amepona maumivu yake na anaweza kuwepo katika kikosi cha kwanza lakini uchaguzi wa kikosi cha kwanza wa meneja Mourinho utategemea na mchezo makosa ya mchezo wa Ukraine.
Spurs inakumbuka ushindi wa goli 3-0 mwezi Aprili magoli ya kipindi cha pili yakifungwa na Dale Alli, Alderweireld na Lamela.
Tamwimu za matokeo kuanzia msimu wa 2009/10 hadi msimu uliopita zinaonyesha kuwa Manchester United imeshinda mara 7 na Spurs ikishinda mara 3 katika michezo 10.
Anfiled
Liverpool vs West Ham
Liverpool vs West Ham
- Liverpool iliyo katika nafasi ya 3 kwa matokeo ya ushindi mara 9 kufungwa mara 2 na sare 3 ikiwa na alama 30 itakuwa ikijaribu kupata ushindi na kurejea katika utaratibu wao mzuri wa ushindi msimu huu watakapokuwa wakikabiliana na wagonga nyundo West Ham United FC wenye ushindi wa michezo 3 kufungwa michezo 8 na kwenda sare mara 3 wakiwa na alama 12 katika mchezo mwingine wa wiki ya 15 ya Premier League uwanja wa Anfield Jumapili.
Liverpool imepoteza mbele ya Bournemouth katika dimba la Vitality kwa kufungwa goli 4-3 kama ilivyo kwa West Ham waliopoteza mbele ya Arsenal kwa kipigo cha 5-1 katika uwanja wa nyumbani London Stadium.
Team News
Liverpool itakuwa na nguvu ya mlinzi kitasa Joel Matip baada ya kukosekana katika mchezo dhidi ya Bournemouth ambapo alikuwa akiuguza maumivu ya enka.
Kuna nafasi nzuri kwa Adam Lallana kuanza baada ya kuliacha benchi wikiendi iliyopita.
Sadio Mane ambaye aliumia katika mchezo dhidi ya Bournemouth ametajwa kuwa yuko fiti kucheza mchezo wa hapo kesho.
Daniel Sturridge hatahusika katika mchezo huo.
West Ham imekuwa ina majeruhi kadhaa ambao wamekuwa wakikiweka katika wakatim mgumu kikosi cha wagonga nyundo msimu huu.
West Ham imekuwa katika wakati mgumu katika kutengeneza kikosi cha kwanza.
Aaron Cresswell na Michail Antonio wanakaribia kuponya maumivu na kurejea kikosini, lakini haiko wazi kama watahusika katika mchezo dhidi ya Liverpool.
0 comments :
Post a Comment