Cairo,Misri.
MIAMBA wa soka wa Misri,Al Ahly wameendeleza umwamba wao kwenye ligi kuu ya nchi hiyo baada ya Jumatu usiku kutwaa ubingwa wao wa 39 kufuatia kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 na wapinzani wao ambao pia wanashika nafasi ya pili Misr El-Maqasa huku ligi ikibakiza michezo minne kufika mwisho.
Ubingwa huo ambao ni wa 10 katika kipindi cha miaka 11 unaifanya Al Ahly ikae kileleni kwa tofauti ya pointi 12 dhidi ya wapinzani wao Misr El-Maqasa wanaoshika nafasi ya pili.
Ikumbukwe hata kama Misr El-Maqasa watashinda michezo yao yote iliyobaki na Al Ahly kufungwa bado matokeo hayo hayatabadili sura ya msimamo kwani sheria ya head-to-head inaibeba Al Ahly kwa kuwa ilishinda mchezo wao wa kwanza.
Katika mchezo wa jana Jumatatu usiku uliochezwa kwenye uwanja wa jeshi wa Suez's Army Stadium,mabao ya Al Ahly yalifungwa na Junior Ajayi na Walid Soliman huku mabao ya Misr El-Maqasa yakifungwa na Ahmed El Sheikh na John Antwi wanaochezea timu hiyo kwa mkopo wakitokea Al Ahly.
0 comments :
Post a Comment