
CHELSEA chini ya kocha mpya Antonio Conte inazidi kuwa tishio kwenye Premier League baada ya kuichapa timu ngumu ya Tottenham 2-1 na kurejea kileleni. Tottenham ilikuwa ya kwanza kuandika bao la kuongoza kunako dakika ya 11 kupitia kwa Christian Eriksen, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa Chelsea kuruhusu goli katika mechi sita zilizopita za Ligi Kuu. Chelsea wakasawazisha dakika ya mwisho kabla ya mapumziko mfungaji akiwa ni Pedro Rodriguez huku Victor Moses akitupia la ushindi dakika ya 52. Chelsea: Courtois, Azpilicueta, Luiz, Cahill, Moses (Ivanovic), Kante, Kante, Matic, Alonso, Pedro (Oscar), Costa, Hazard (Willian) Begovic, Fabregas, Batshuayi, Chalobah Tottenham: Lloris, Walker, Dier, Vertonghen, Wimmer, Wanyama, Dembele (Janssen) , Eriksen, Alli (Nkoudou), Son (Winks), Kane Victor Moses akishangilia bao la ushindi la Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge
0 comments :
Post a Comment