ARSENAL imekuwa chaguo bora zaidi kwa kiungo wa Ujerumani Sami Khedira dhidi ya Chelesea baada ya magaezi nchini Hispania kuripoti kuwa mpango wa uhamisho wa pauni milioni 23 kutoka Real Madrid kwenda Emirates umeafikiwa
.
Kwa mujibu wa gazeti la Sport, Khedira atasaini mkataba wa miaka minne Arsenal licha ya Chelsea kuonyesha utashi wa kutaka saini yake.
Mazungumzo ya mkataba mpya baina ya wawakilishi wa staa huyo mwenye umri wa miaka 27 na Real Madrid yalivunjika na sasa wanaona ni bora kumpiga bei kuliko kumwacha aondoke bure msimu ujao.
Bosi wa Chelsea Jose Mourinho ambaye alifanya kazi na Khedira wakati alipokuwa akiikochi Real Madrid, alimtaka sana kiungo huyo mkabaji lakini sasa anaonekana wazi kumkosa.
Khedira alikosa mechi ya fainali baada ya kuumia mwenyewe wakati wa kupasha mwili moto muda mfupi kabla ya mchezo kuanza, lakini alijumuika na wachezaji wenzake uwanjani kushangilia ubingwa.
0 comments :
Post a Comment