Ujerumani
watakutana na Argentina kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia 2014
hapo baadae leo kwenye dimba la Maracana, Brasilia.
MWANA SPORT LEO inakuletea
fomesheni tarajali katika mchezo huo, line-ups na maelezo mafupi ya
kila mchezaji ambaye ataanza kwenye kikosi cha kwanza katika timu yake,
pamoja na makocha.
Mlinda mlango: Manuel Neuer, Bayern Munich (28)
Kombe la Dunia 2014: Manuel Neuer aliokoa mpira uliokuwa wa kusawazisha dhidi ya Ufaransa.
Mashindano haya yamemsaidia Manuel Neuer kuonesha ubora wake na kumfanya atajwe kuwa mlinda mlango namba moja duniani.
Wachambuzi
wa masuala ya soka wanampa heko kutoka na uwezo wake wa kupangua
michomo ya hatari na uthubutu wake kutoka langoni ili kuokoa hatari.
Ameokoa hatari 21 nje ya eneo lake la 18 katika mchezo dhidi ya Algeria.
Amepoteza michezo mitatu pekee katika michezo 51 aliyoichezea Ujerumani.
Je, unajua? Ni mlinda mlango wa Costa
Rica Keylor Navas pekee ambaye ameweka rekodi ya kuokoa kwa 91.3% zaidi
ya Neuer mwenye 85.2% kwenye Kombe la Dunia mwaka huu.
Beki wa kulia: Philipp Lahm, Bayern Munich (30)
Akielezewa
na kocha wa klabu Pep Guardiola kama "mchezaji mwenye akili kuwahi
kumfundisha", matokeo yake yameonekana kwenye Kombe la Dunia la mwaka
huu ambapoamekuwa na uwezo wa kutoka kwenye nafasi yake ya beki wa kulia
hadi kucheza kwenye nafasi ya kiungo mkabaji kama ambavyo amekuwa
akifanya kwenye klabu yake ya Bayern Munich pale anapohisi kuna
uwezekano wa kufanya hivyo hasa wakizidiwa, lakini Ujerumani imekuwa na
ngome ngumu ya ulinzi kuliko ushambuliaji tangu pale aliporejea kwenye
nafasi ya full-back kwenye mchezo wa robo fainali. Mchezo wa fainali
utakuwa ni mchezo wake wa 20 wa Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani.
Je, wajua? Hakuna mchezaji mchezaji yeyote aliyepiga pasi fupi zaidi ya Lahm kwenye fainali hizi (450).
Mlinzi wa kati: Jerome Boateng, Bayern Munich (25)
Wakati
mashindano haya yanaanza, alichezeshwa kama mlinzi wa kulia lakini
akahamishwa hadi mlinzi wa kati kwa sababu ya kuungana na majeruhi na
Lahm akarejeshwa nyuma. Aliumia mara mbili mapema katika mashindano
haya, lakini ni mmoja kati ya wachezji wanaounda kikosi cha kwanza cha
Joachim Low. Alikutana na kaka yake, Kevin-Prince wa Ghana, kwenye
mchezo wao wa hatua ya makundi katika fainali ya pili mfululizo.
Je, wajua? Ameanza kwenye kila mchezo katika michezo 11 ya mwisho ya Ujerumani kwenye Kombe la Dunia.
Mlinzi wa kati: Mats Hummels, Borussia Dortmund (25)
Hakuwa
na uhakika wa kuanza kwenye kikosi cha kwanza akiwa kama mlinzi wa kati
kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia, ni miongoni mwa walinzi
wanaopigania namba katika kikosi cha Ujerumani, lakini akijivunia nguvu
zake ambazo zinamfanya aweze kumudu nafasi hiyo. Hakika, mlinzi huyo wa
Borussia Dortmund amekuwa silaha muhimu, akifunga mara mbili kwa kichwa
katika michezo dhidi ya Ureno na Ufaransa. Wakati wote huu alikuwa
katika vita vikali vya kuugua mafua.
Je, wajua? Mama yake alikuwa mwanamke wa kwanza kutangaza mpira wa miguu kwenye Televisheni ya Ujerumani.
Beki wa kushoto: Benedikt Howedes, Schalke (26)
Ni
beki wa kati katika klabu yake ya Schalke, ameisaidia kwa kiasi kikubwa
Ujerumani kuziba pengo la mlinzi wa kushoto. Mchezaji mwenye kila kitu
katika mashindano haya, ameanza katika kila mechi kwenye fainali za
Brazil ambapo kocha Low alianza na masentahafu wanne. Kabla ya Kombe la
Dunia kuanza alikuwa ndani ya gari aina ya Mercedes lililopata ajali
iliyomuhusiaha dereva wa F1 Nico Rosberg, lakini hakuumia.
Je, wajua? Howedes amezuia mara nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote wa Ujerumani katika fainali hizi za Kombe la Dunia (15).
Kiungo wa kati: Sami Khedira, Real Madrid (27)
Aliifungia Ujerumani bao la tano katika mchezo dhidi ya wenyeji Brazil.
Baada ya kuumia goti mwezi Novemba, ushiri wa Khedira kwenye Kombe la Dunia ulionekana kufififa.
Lakini
yoyote ambaye alimtilia mashaka Joachim Low kuwa na imani kwamba kiungo
huyo wa Real Madrid angeweza kucheza kwenye mashindano haya, lazima
ataona aibu kutokana na kiwango kizuri alichokionesha kwenye mchezo
dhidi ya Brazil.
Tangu
alipoanza kuchezeshwa sambamba na Bastian Schweinsteiger, kiungo mwenza
tangu fainali za mwaka 2010, katika mchezo wa robo fainali, Ujerumani
imekuwa ikionekana imara zaidi na tishio.
Je, wajua? Khedira aliweka rekodi ya kutengeneza goli na kufunga kwenye Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya Brazil.
Kiungo wa kati: Bastian Schweinsteiger, Bayern Munich (29)
Baada
ya majeruhi ambayo yalishuhudia yakimuweka nje kwenye klabu yake ya
Bayern Munich karibu msimu mzima, aliumia goti wakati wa mazoezi ya
kabla ya Kombe la Dunia wakati wapo kambini na kukaribia kuharibu
maandalizi yake kwenye fainali hizi. Kocha Joachim Low alimuwacha nje
kwenye kikosi kilichoanza mechi mbili za awali, lakini nahodha msaidizi
wa Ujerumani alirejea dimbani kwenye mchezo dhidi ya Brazil katika
nafasi yake na kufanya vizuri.
Je, wajua? Schweinsteiger
ameichezea Ujerumani michezo 19 ya Kombe la Dunia; ni wachezaji watatu
pekee wameicheza Ujerumani mechi zaidi za Kombe la Dunia (Lothar
Matthaus, Miroslav Klose na Philipp Lahm).
Kiungo mshambuliaji: Thomas Muller, Bayern Munich (24)
Mdahalo
unaweza kuibuka juu ya nafasi inayomfaa Muller, lakini anacheza kama
namba tisa ya uongo, mshambuliaji wa kati au mshambuliaji wa pembeni,
bali atafunga magoli daima.
Umri
wake ni miaka 24 na anakaribia kutwaa kiatu cha pili cha dhahabu huku
akisaidiwa na hat-trick katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi dhidi ya
Ureno.
Tayari
ameshaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu katika historia ya Ujerumani
baada ya Teofilo Cubillas na mchezaji-mwenza Miroslav Klose kufunga
mabao matano au zaidi kwenye fainali mbili tofauti za Kombe la Dunia.
Je, wajua? Muller amefunga mabao 10 na kutengeneza sita katika michezo 12 ya Kombe la Dunia.
Kiungo mshambuliaji: Toni Kroos, Bayern Munich (24)
Hujulikana
kwa ukimya wake lakini mwenye kufanya mambo ya uhakika kwenye timu ya
taifa ya Ujerumani na klabu yake ya Bayern Munich, uwezo wake katika
mashindano haya umemfanya awe imara zaidi.
Alifunga
mara mbili dhidi ya Brazil na hayo yalikuwa magoli yake ya kwanza
kwenye fainali za Kombe la Dunia na alikuwa mchezi bora katika mchezo
huo.
Amecheza
michezo yote ila dakika mbili pekee katika michezo sita ya Ujerumani na
huenda akatajwa na nchi yake kuwa mchezaji bora wa mashindano.
Je, wajua? Kroos
amegusa mpira mara nyingi zaidi ya mchezaji yeyote katika fainali hizi
za Kombe la Dunia (606) ikijumuishwa na ile ya kuvutia 135 dhidi ya
Algeria.
Kiungo mshambuliaji: Mesut Ozil, Arsenal (25)
Mchezaji
aliyeweka rekodi ya usajili wa Arsenal bado hajaonekana kuwa na
mafanikio makubwa nchini Brazil, kutokana na walinzi wengi wa Ujerumani,
Paul Breitner anashauri aondolewe kwenye kikosi. Alipoteza nafasi nzuri
ya kuifanya Ujerumani ipate ushindi wa 8-0 dhidi ya Brazil.
Aliandikakwenye ukurasa wake wa Twitter baada ya mchezo wa nusu fainali
ambayo waliishinda Brazil 7-1 kusema kwamba anategemea kipigo
hakijaiathiri Brazil.
Je,
wajua? Hakuna mchezaji yeyote wa Ujerumani aliyetengeneza nafasi nyingi
zaidi kwa mchezaji-mwenza katika fainali hizi zaidi ya Ozil (15).
Mshambuliaji: Miroslav Klose, Lazio (36)
Imeandikwa
kwenye nyota kwamba Klose atakuwa mfungaji bora wa muda wote wa Kombe
la Dunia baada ya kumzidi nyota wa Brazil Ronaldo, dhidi ya Wabrazil,
nchi Brazil.
Alipofunga kwa ufundi katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya wenyeji, ilimaanisha kwamba sasa ana magoli 16 ya Kombe la Dunia.
Anaongoza
kwa ufungaji Ujerumani akiwa na magoli 71 kwenye michezo 136, ni
mchezaji wa tatu kufunga katika fainali nne za Kombe la Dunia na
Ujerumani haikuwahi kupoteza mchezo ambao Klose amefunga.
Je,
wajua? Amecheza michezo 23 ya Kombe la Dunia ambayo inamfanya kuwa
katika nafasi ya pili kuwa mchezaji wa muda wote aliyecheza michezo
mingi ya Kombe la Dunia nyuma ya Paolo Maldini, na Lothar Matthaus waliocheza michezo 25.
Kocha: Joachim Low (54)
Hawezi
kuelezewa kama mchezaji, lakini msaidizi huyo wa zamani wa Jurgen
Klinsmann amesaidia kwa kiwango kikubwa kulibadilisha soka la Ujerumani
kutoka soka lisilovutia hadi kuwa soka la burudani miongoni mwa timu za
taifa ulimwenguni. Hivyo, baada ya kupoteza katika nusu fainali au
fainali katika fainali tatu za Kombe la Dunia, huenda presha ikaongezeka
kama atarudi mikono mitupu tena.
Mlinda mlango: Sergio Romero, Sampdoria (27)
Nafasi ya mlinda mlango ilikuwa ni tatizo katika kikosi cha Argentina wakati wakijiandaa kwenye mashindano haya.
Lakini baada ya yote, Romero amefanya kila aliloweza akicheza kwa mkopo kwenye klabu ya Monaco msimu uliopita.
Bila
shaka, kipa huyo, 27 amefungwa mabao matatu katika mechi sita nchini
Brazil na kuokoa mara mbili huku akiisaidia nchi yake kutinga hatua ya
fainali dhidi ya Uholanzi.
Je, wajua? Romero ni mlinda mlango wa kwanza wa Argentina kucheza michezo minne bila kufungwa kwenye Kombe la Dunia.
Beki wa kulia: Pablo Zabaleta, Manchester City (29)
Beki
kisiki wa Manchester City alikosa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010
lakini amekuwa mchezaji muhimu katika safu ya ulinzi ya Argentina nchini
Brazil. Zabaleta, 29 alipost picha yake baada ya mchezo wa nusu fainali
akivaa wigi la blue na bendeji akizuia sehemu ambao aliumia baada ya
kukumbana na Dirk Kuyt.
Je, wajua? Zabaleta
amepiga pasi nyingi katika moja ya tatu ya fainali za Kombe la Dunia
mwaka huu zaidi ya mlinzi yeyote wa Argentina (64).
Mlinzi wa kati: Martin Demichelis, Manchester City (33)
Mchezaji
mwingine wa Manchester City akiwa katika jezi za timu yaifa kwa ajili
ya fainali ya Kombe la Dunia. Umri wake ni miaka 33 hakuwa na athari
katika hatua ya makundi wala katika mchezo wa mtoano dhidi ya
Switzerland. Alianza kwenye kikosi cha kwanza katika michezo miwil
iliyopitasanjari na Ezequiel Garay na akaonekna kuwa na umuhimu na
huenda akaanza tena kesho kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumani.
Je, wajua? Demichelis alitibua mara nane kwenye mchezo dhidi ya Uholanzi, mara tano zaidi ya mchezi yeyote wa Argentina.
Beki wa kati: Ezequiel Garay, Zenit St Petersburg (27)
Alikaribia
kujiunga na Manchester United msimu uliopita, Garay aliumia jicho
kwenyemchezo wa nusu fainali dhidi ya Uholanzi wakati alipokuwa
akijiweka sawa wakati akifunga moja ya kiatu chake mikononi. Kama
Zabaleta, aliumia kichwani kwenye mchezo dhidi ya Uholanzi lakini wakati
huu akikumbana na mlinzi-mwenza Ron Vlaar.
Je, wajua? Ameokoa kwa kichwa mara nyingi zaidi (36) kuliko mchezaji yeyote wa safu ya ulinzi ya Argentina.
Beki wa kushoto: Marcos Rojo, Sporting Lisbon (24)
Mlinzi
wa Sporting Lisbon amecheza chicni ya kocha Alejandro Sabella katika
klabu ya Estudientes nchini Argentina. Alihusishwa na kutaka kuhamia
katika klabu za Liverpool na Chelsea na alikuwa miongonimwa wafungaji
nchini Brazil wakai alipofunga katika mchezo wa hatua ya makundi dhidi
ya Nigeria, akiunganisha free-kick kwa goti lake.
Je, wajua? Rojo
amekaba mara nyingi zaidi ya mlinzi yeyote wa Argentina (17), na
kutengeneza nafasi nyingi zaidi kutoka nafasi ya ulinzi (7).
Kiungo wa kati: Javier Mascherano, Barcelona (30)
Anatofautiana
sana na Lionel Messi lakini nakubalika zaidi na timu yake, umuhimu wake
ulionekana zaidi pale alipoweza kumzuia Arjen Robben ili asifunge
katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia. Kiungo wa zamani wa
Liverpool, ambaye alikuwa muhimu pia katika fainali za Kombe la Dunia
mwaka 2010, ni kiungo mkabaji - licha ya kucheza nafasi ya beki katika
klabu yake ya Barcelona.
Je, wajua? Javier Mascherano amepiga pasi za mbali 509 na amezuia mara 28.
Kiungo wa kulia: Lucas Biglia, Lazio (28)
Umri
wake ni miaka 28 na anakipiga katika klabu ya Lazio nchini Italia,
alianza katika kila mchezo miongoni mwa michezo minne ya awali katika
mashindano haya, na alitolewa katika kila mchezo na huenda akapangwa
kwenye kiungo wa kulia katika mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumai.
Kiungo huyo alianza katika michezo miwili ya mwisho.
Je, wajua? Lucas
Biglia lipiga pasi zilizokamilika kwa 90% katika mchezo dhidi ya
Uholanzi, ni kiwango kikubwa kwa kiungo wa Argentina kufanya hivyo.
Kiungo wa kushoto: Enzo Perez, Benfica (28)
Anajulikana
kama mpambanaji na mwenye bidii, kiungo wa Benfica ni mchezaji ambaye
ana kila sifa na tayari anahusishwa na kutaka kuhamia Manchester United.
Majeruhi ya Angel Di Maria yalimpa nafasi ya kuanza kwenye mchezo dhidi
ya Uholanzi na hakumuangusha kocha wake. Alikuwa mchezaji bora wa mwaka
kwenye Ligi ya Ureno msimu uliopita.
Je, wajua? Enzo Perez amemaliza dakika 90 mara moja katika michezo 10 aliyoichezea Argentina (v Slovenia).
Fowadi: Gonzalo Higuain, Napoli (26)
Jina
lake la utani ni Pipita, mshambuliaji wa Napoli alifunga hat-trick
pekee katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 na alikuwa nafasi ya
tatu nyuma ya Messi na Luis Suarez kwa magoli wakati wa kufuzu kwa
upande wa nchi za Amerika ya Kusini.
Alitokea benchikwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Bosnia-Hercegovina na akatoa pasi iliyozaa bao la ushindi kwa Messi.
Alifunga goli pekee kwenye ushindi wa robo fainali dhidi ya Ubelgiji.
Je, wajua? Higuain
amefunga magoli pungufu katika fainali za mwaka huu zaidi ya zile za
2010 licha ya kucheza michezo miwili zaidi (goli moja 2014, magoli manne
2010); akipiga mashuti machache katika fainali hizi pia (mashuti 10
mwaka huu, 13 2010).
Fowadi: Lionel Messi, Barcelona (27)
Mchezaji
bora wa mechi nne katika michezo minne ya timu yake na kufunga magoli
manne pia likiwemo goli safi dhidi ya Bosnia-Hercegovina na Iran.
Alifunga
mara mbili kwenye mchezo dhidi ya Nigeria na fowadi huyo kuonesha
ishara kwamba anastahili kuwa mchezaji bora wa Dunia kwa kutawala pia
Kombe la Dunia.
Laki, Messi, 27 hakuwa muhimu sana kwenye mchezo dhidi ya Uholanzi na alitajwa kuwa huenda ndito mwisho wake.
Je, wajua? Lionel Messi ametengeneza nafasi 21 katika mashindano haya, zaidi ya mchezaji yeyote katika fainali hizi.
Fowadi: Ezequiel Lavezzi, Paris St-Germain (29)
Alitaka
kuachana na masuala ya soka ili awe fundi umeme baada ya kukataliwa na
klabu ya Boca Juniors akiwa na umri wa miaka 16, Lavezzi ni mmoja kati
ya wachezaji muhimu wa Argentina kwenye fainali hizi. Ana tattoo ya
Diego Maradona katika paja lake la kushoto - mtu aliyemuwacha kwenye
kikosi cha Argentina kilichoshiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka
2010. Alionekana akitema maji uelekeo wa kocha wake Alejandro Sabella
wakati wa mchezo dhidi ya Nigeria.
Je, wajua? Lavezzi amepiga mashuti mawili pekee kwenye fainali hizi, ni chache kuliko fowadi yeyote wa Argentina.
Kocha: Alejandro Sabella (59)
Aliwahi kuwa kocha wa Sheffield United na Leeds United, Sabella ameonesha mafanikio zaidi kuliko mtangulizi wake Diego Maradona.
Anaonekana
kama mwalimu wa shule lakini mzee huyo wa miaka 59 amekuwa na mafanikio
nchini Brazil na anatarajia kuijenga timu iliyojaa vipaji zaidi
wakiongozwa na Messi kwenye mchezo wa fainali hapobaadae leo
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment