News
Loading...

MALIMI BUSUNGU APATA AJALI MBAYA YA GARI !! HABARI ZOTE HAPA!!

Taarifa za mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu zimezidi kuzagaa na imeelezwa amepata ajali ya gari akiwa njiani kwenda Dodoma.

Awali kulikuwa na taarifa mbaya kwamba alipoteza maisha lakini baadaye zikathibitika ni za uzushi.

Juhudi za kumpata zilikuwa ngumu, baadaye meneja wake akathibitisha alipata ajali.

“Kweli kapata ajali, gari imeharibika sana. Niliwapigia akapokea mtu simu yake na kuthibitisha, lakini amesema Malimi yuko poa,” alisema.

Baadaye, SALEHJEMBE ilipiga simu ya Busungu, alipokea na kuthibitisha ajali hiyo lakini akasema bado yuko polisi anaandikisha.


“Bado naandikisha hapa, halafu tutazungumza,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment