LAZAR Markovic mshambuliaji kutoka Benfica ya Ureno amewasili Merseyside kufanya vipimo vya afya na anatarajiwa kuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Liverpool ndani ya saa 24 zijazo.
Nyota huyo wa kimataifa wa Serbia alipaa siku ya Jumapili jioni kuelekea Liverpool na tayari ameanza kufanyiwa vipimo vya afya katika Hospitali ya Spire Liverpool na kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, Melwood kabla hajakamilisha usajili wake wa pauni milioni 20.
Kama kila kitu kitaenda vizuri kwenye vipimo vyake vya afya, Markovic ambaye atasaini mkataba wa muda mrefu, anatarajiwa kutangazwa rasmi kama mchezaji wa Liverpool ndani ya saa 24.
Usajili wa mshambuliaji huyo wa kushoto unafuatia ule wa awali wa Rickie Lambert, Adam Lallana na Emre Can huku mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi naye akiwa anakaribia kujiunga na Liverpool, ambayo inaendelea kumsaka beki wa kushoto wa Sevilla Alberto Moreno.
0 comments :
Post a Comment