LUIZ Felipe Scolari amesema hatajiuzulu katika nafasi yake ya ukocha wa timu ya taifa ya Brazil, licha ya timu yake kufungwa mara ya pili mfululizo ndani ya siku tano.
Brazil walifungwa mabao 7-1
katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa Belo Horizonte siku ya jumanne
ya wiki hii na usiku wa jana walifungwa mabao 3-0 na Uholanzi na
kumaliza katika nafasi ya nne ya fainali za 2014 za kombe la dunia
kwenye ardhi yake.
Kabla ya mashindano haya, Brazil
ilikuwa haijapoteza mechi nyingi za nyumbanii tangu mwaka 2002 na
walikuwa hawajawahi kufungwa nyumbani katika mashindo ya mpira wa miguu
tangu mwaka 1975, lakini kufungwa mara mbili mfululizo ndani ya siku
tano kumewachangaya mashabiki na waandishi wa habari wan chi hiyo.
Lakini Scorali alikutana na
waandishi wa habari baada ya kufungwa na Uholanzi na kusisitiza kuwa
shirikisho la soka nchini Mbrazil litaamua hatima yake ya baadaye.
“Ulikuwa mchezo wenye nguvu
sawa,” alisema. “Wachezaji wanatakiwa kupongezwa kwa jinsi walivyocheza.
Hatukucheza vibaya-hayo ndio maoni yangu”.
“Kwasasa sio muda muafaka wa
kuzungumzia hilo, “ alisema Scolari. “Nitaandika ripoti yangu na
kumwambia rais wa CBF ni kitu gani nadhani hakikwenda sawa, yeye ataamua
nini anataka kwa baadaye. Tumepoteza mechi nyingine, lakini maisha
yanaendele”.
“Mwaka mmoja uliopita nilishinda
kombe la mabara,” aliongeza. “Makosa hayako kwa makocha. Kitu ni kwamba
tuna timu ya vijana sana. Hatujazalisha wachezaji wa kutosha, kwahiyo
sio kazi rahisi hata kama Kocha mwinine atakuja”
0 comments :
Post a Comment