Messi anakosolewa na wadau wa soka kwamba ameshindwa
kuonesha kiwango chake cha Barcelona katika soka la kimataifa, lakini
amefanya kazi kubwa kuifikisha Argentina katika fainali ya leo usiku
dhidi ya Ujerumani.
“Ni mtu wa ajabu,” Beckham alisema kwenye mahojiano na chaneli ya Adidas football ya YouTube.
“Anawapa watu presha kubwa kwa
aina yake ya uchezaji na kitu kinachompa upekee ni kuweza kucheza kama
wenzake, ni mchezaji wa timu”.
“Amepata uwezo binafsi mkubwa,
lakini ushindi unamaanisha kila kitu kwake. Kama wachezaji wenzake
wanafunga mabao, anakuwa wa kwanza kushangilia nao na nadhani ile ina
maana kubwa kuhusu yeye”
“Kucheza na Argentina, nina
uhakika kuna presha kiasi fulani ukiangalia huko walikotoka. Kushinda
ina maana kubwa kwake, familia na kila mmoja anayemzunguka duniani”.
Akiwa mgumu kutoa utabiri wake
kuhusu mechi ya fainali, Beckham-ambaye atakuwepo kwenye mchezo akiwa na
watoto wake, hatimaye aliweka wazi utabiri wake na kusema Argentina
itashinda mabao 3-1.
Alisema: “Inashangaza kuwa timu hizi mbili zimekutana pamoja”.
“Ujerumani walikuja kwenye
michuano wakiwa na uzoefu mkubwa, watu hawajashangaa kuona wamefika
hatua hii. Hakuna mchezaji mmoja nyota, wana kundi kubwa la wachezaji
wanaocheza pamoja”.
“Argentina ina kundi la
wachezaji wenye vipaji, ambao wanacheza kwa mapenzi makubwa, lakini
Lionel, ninafurahia kumuona anacheza.
0 comments :
Post a Comment