News
Loading...

IMANI YA MESSI, WAARGENTINA WAJAZANA BRAZIL KUBEBA KOMBE


Brazil inaweza kujaa Waargentina kwa kuwa tokea juzi wameanza kuwasili kwa wingi nchini humo. Lengo ni kushangilia ushindi wa Kombe la Dunia.

Usisahau Argentina leo wanauvaa 'mkwaju' Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia.
Wengi wao wameamua kwenda kwa wingi nchini Argentina kwa kuwa tu wanamuamini Lionel Messi, nyota wao wanayeamini anaweza kufanya lolote.

Kutoka Kusini mwa Argentina katika eneo la Tierra del Fuego, nenda hadi mji mkuu wa capital Buenos Aires hadi mji aliozaliwa Messi wa Messi wa Rosario, wamefunga safari kwa wingi na sasa wako Rio de Janeiro.

Idadi kubwa ya mashabiki hao wakiwa kwenye Coaster, vipanya na gari ndogo za kizamani, wameingia Brazil wakiwa na shangwe ya kutosha kwa kuwa tu wanamuamini Messi atafanya maajabu na kuwang’oa Wajerumani leo, ubingwa uende Argentina.
Mashabiki hao wanalazimika kuendesha gari kwa siku mbili kutoka Buenos Aires hadi Sao Paulo.
Ukiachana na njia za barabara, ndege zote za kutoka Argentina kwenda Brazil zimejaa topu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment