News
Loading...

SOMA MAKALA HII YA KUSIKITISHA YA JAMAA ALIVYOKOMAA MPAKA SASA ANAKWENDA KUANDIKA HISTORIA KUBWA KATIKA MAISHA YA SOKA


DAKAR, SENEGAL. MAISHA hayataki mchezo mchezo. Kuwa na maisha bora kunahitaji kuwa na uthubutu. Mamadou Coulibaly anasubiri kuandika historia kubwa kabisa katika maisha yake kutoka kuwa mtoto mkimbizi hadi kujiunga na moja ya klabu maarufu duniani katika mchezo wa soka.
Coulibaly (18) kwa sasa ni kiungo matata kabisa katika kikosi cha Pescara kilichokuwa kikicheza Ligi Kuu Italia msimu huu, kabla ya kushuka daraja kutokana na kuwa mkiani. Lakini, kwa namna alivyotoka kwao Senegal hadi kuingia Ulaya, ndicho kitu kinachotoa tafsiri kwamba maisha yanahitaji kupambana.

Mambo magumu yote aliyokumbana nayo katika safari yake ya kutoka Senegal hadi Ulaya yanakaribia kuleta matunda baada ya kuwa katika hatua za mwisho kabisa kukamilisha usajili wa kujiunga na mabingwa wa Italia, Juventus.

Stori ya maisha ya Coulibaly yanatoa funzo kwamba, hupaswi kukata tamaa bila ya kujali vikwazo gani umekuwa ukikumbana navyo kwenye harakati za jambo lolote unalotaka kulifanya.

Coulibaly, ambaye siku si nyingi atakuwa staa mkubwa duniani, aliingia Ulaya mwaka 2015 baada ya safari ya misukosuko mingi kutoka Senegal, akapitia Morocco kabla ya kufika kwa Wazungu na kisha kipaji chake cha mpira kilionekana na Pescara.

Anasimulia jinsi alivyojivika ujasiri na kuondoka nyumbani kwao bila ya kuaga, akiwa amebeba kibegi chake tu mgongoni na kwenda Ulaya kwa njia za panya. “Niliondoka nyumbani na kibegi changu cha mgongoni.

“Nilimwambia Mamadou tu, huyu ni rafiki yangu na wazazi wangu walidhani nipo shule.

Nilizima simu na sikupiga simu yoyote kwa miezi mitano au minne hivyo, walidhani nimekufa.

“Nyumbani kwetu hakukuwa na shida, tulikuwa na chakula cha kutosha tu kwa sababu watoto tulikuwa mimi na dada zangu wawili. Baba yangu hakutaka kabisa nicheze soka. Kwake yeye shule ndiyo ilikuwa kitu cha muhimu, mimi natokea kwenye familia ya walimu.

“Baba aliniambia atanipeleka kwenye timu za Ulaya, lakini alifanya hivyo kunituliza tu. Nikaamua kuyaweka hatarini maisha yangu kwa ajili ya soka, lakini nimefanya hivyo kwa ajili yao, siku si nyingi nitaanza kuwasaidia,” anasema Coulibaly.

Kwa maneno hayo unaweza kuona kumbe Coulibaly alipata mambo kirahisi rahisi tu, lakini yalikuwa magumu sana. Coulibaly alikuwa akilala mitaani na angepoteza hata maisha baada ya boti aliyokuwa akisafiria kuingia Ulaya kupata matatizo na hakuwa akiweza kuogelea.

“Nililipia tiketi ya basi kutoka Dakar hadi Morocco, hilo halikuwa tatizo, tatizo lilikuja baadaye.

USIKOSE KESHO UJUE SFARI YAKE ILIKUJE!!
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment