News
Loading...

DUUH!! MWIGULU NGOJA HAJI MANARA AKUSIKIE UTAJUTA KUMFAHAMU!! HEBU SOMA MADONGO YA MWIGULU NA SAMAHANI ZAKE KWA YANGA


MDAU wa Yanga, Mwigulu Nchemba, ambaye sasa ameamua kuelekeza nguvu katika timu ya nyumbani kwao, Singida United, amesema kwa jinsi wanavyojitapanga ni ndoto kwa Simba kutwaa ubingwa msimu ujao.
Mwigulu ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba, alitoa kijembe hicho juzi wakati akizungumza kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika vijiji vya Mlandala,Urughu na Ndago jimboni kwake.

“Juzi juzi waliponyakua kakombe kadogo pale Dodoma, walifurahi kupitiliza. Kakombe hako kalikata kiu waliyokuwa nayo ya kukosa makombe kwa kipindi kirefu cha miaka minne,”alisema Mwigulu.

“Niwaambie tu watani zangu Simba kuwa wataendelea kuukosa ubingwa wa ligi kuu kwa miaka mingine mingi ijayo. Msimu ujao nimehamishia nguvu zangu nyumbani kwenye timu ya Singida United ambayo tunatarajia itakuwa bingwa ligi kuu msimu ujao,” alifafanua.

Ametumia fursa hiyo kuiomba radhi timu yake ya Yanga, kwa madai kwamba msimu ujao wa ligi kuu, atahamishia nguvu zake Singida United, kuhakikisha kwa mara ya kwanza inaleta kombe la ubingwa kanda ya kati.

Katika hatua nyingine, Mwigulu amesema wameandaa programu ya kukusanya vijana wadogo wazawa wenye vipaji vya kucheza soka na kuahidi kukuza vipaji hivyo,lengo likiwa ni kupunguza tatizo la kusajili wachezaji nje ya mkoa.

“Mkakati ni kuwa na wachezaji watakaotanguliza uzalendo mbele na kuutangaza vizuri mkoa wao wa Singida,” alisema.

“Pia wao binafsi watakuwa na malengo ya kutangaza majina yao ili kujijengea mazingira mazuri.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment