News
Loading...

DIDA AITIA YANGA MABEGANI MWAKE AIBEBA MPAKA NUSU FAINALI


Dar es Salaam. Yanga imefuzu kwa nusu fainali ya Kombe la SportPesa kwa kuifunga Tusker kwa penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 kwa suluhu.
Kipa wa Yanga, Deogratius Munishi 'Dida' amethibisha ubora wake baada ya kupangua penalti mbili na kuhakikishi timu yake kufuzu kwa nusu fainali dhidi ya AFC Leopards iliyoitoa Singida United kwa penalti 5-4.
Nyota ya kipa wa Yanga, Munishi iling'ara baada ya kupanga penalti ya Clifford Alwanga huku Stephen Owusu akipaisha.
Waliofunga penalti za Yanga ni nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro',  Obrey Chirwa, Said Mussa na Maka Mwakalukwa, wakati walipata kwa upande wa Tusker ni Noah Wafula na Brian Osumba.
Katika mchezo huo Yanga na  Tusker kila moja ilijaribu kucheza kwa kujilianda na kushambulia kwa kushtukiza.
Yanga ilitawala mpira kipindi cha kwanza huku
ikipoteza nafasi kadhaa kupitia kwa mshambuliaji wake Obrey Chirwa na Pato Ngonyani.  
Mabingwa wa Kenya, Tusker ilifanya mashambulizi mengi langoni mwa Yanga, lakini uimara wa safu ya ulinzi wa mabingwa Tanzania Bara ukiongozwa na kipa Munishi 'Dida ulifanya mechi hiyo kumalizika dakika 90 kwa suluhu.
Katika mchezo huo Yanga ilitumia mseto wa wachezaji wake wa timu ya vijana na wakongwe wakiongozwa na Nadir Haroub Cannavaro.
Singida yaaga mapema
AFC Leopards imekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa nusu fainali ya mashindano ya SportPesa kwa kuifunga Singida United  penalti 5-4. baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare 1-1 kwenye Uwanja wa Uhuru.
Katika mchezo huo Singida United ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa dakika ya 10 na Kutinyu  Tafadzwa, kabla ya miamba ya Kenya, AFC Leopards kusawazisha katika dakika ya 63, kupitia kwa Vicent Oburu.
Waliofunga penalti kwa Singida United ni Atupele Green,  Shango Hamis,  Nhivi Simbarashe na Muroiwa Elisha wakati Chuku Salum akipaisha.
Waliofunga penalti kwai AFC ni Bernard Mangoli,  Marselas Ingotsi,  Kateregga Allan,  Duncan Otieno na Fiamenyo Gilbert.
Kocha wa Singida United, Hans Pluim ameanza vibaya kibarua chake baada ya kutupwa nje mashindano ya Sport Pesa.
Mashindano hayo yataendelea kesho Jumanne kwa  Jang'ombe itachuana na Gor Mahia ilihali Simba itavaana na Nakuru All Stars.
 Nusu fainali itafanyika Alhamisi Juni 8 wakati fainali yake itakuwa Jumapili Juni 11 kumpata bingwa atakayecheza na Everton.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment