Hat trick ya Jamie Vardy imewapa Mabingwa Watetezi wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, Leicester City, ushindi wa Bao 4-2 walipocheza na Manchester City Uwanjani King Power.
Leiocester waliongoza 2-0 ndani ya Dakika 5 za kwanza na kuwa 3-0 mbele ndani ya Dakika 20 na Bao hizo kudumu hadi Haftaimu.
Kipindi cha Pili Leicester walifunga Bao lao la 4 na kuwa 4-0 mbele.
Mwishoni, Frikiki ya Aleksandar Kolarov na Bao la Nolito liliwapa City Bao za 2.
+++++++++
MAGOLI:
Leicester City 4
Vardy (3', 20' & 78')
King (5')
Manchester City 2
Kolarov (82')
Nolito (90')
+++++++++
Ushindi huo umeondoa ukame wa Magoli wa Mechi 10 za EPL kwa Straika Jamie Vardy na pia kuipa ushindi wa kwanza Leicester katika Mechi 4 za Ligi na kupanda hadi Nafasi ya 14.
Kwa City hiki ni kipigo chao cha Pili mfululizo na wanabaki Nafasi ya 4.
VIKOSI:
Leicester City (Mfumo 4-4-2): Zieler; Simpson, Huth, Morgan, Fuchs; Mahrez, Amartey, King, Albrighton; Vardy, Slimani.
Akiba: Hamer, Chilwell, James, Mendy, Gray, Musa, Okazaki.
Manchester City (Mfumo 4-1-4-1):Bravo; Zabaleta, Sagna, Stones, Kolarov; Fernando; Navas, Gundogan, De Bruyne, Silva; Iheanacho.
Akiba: Caballero, Sterling, Nolito, Sane, Clichy, Toure, Adarabioyo.
REFA: Michael Oliver
0 comments :
Post a Comment