Henrikh Mkhitaryan (katikati) amepata matumaini mapya Manchester United |
KUFUATIA ushindi wa 4-0 wa Manchester United dhidi ya Feyenoord, Henrikh Mkhitaryan amepata matumaini mapya ya kuwa na nafasi kwenye kikosi cha Jose Mourinho. Hiyo ni baada ya kiungo huyo kung'ara kwenye mchezo huo wa Europa League uliofanyika Alhamsi usiku. Hii ni mara ya pili kwa Mkhitaryan kuanza tangu aliposajiliwa kwa pauni milioni 26 kutoka Borussia Dortmund. Wachambuzi wa soka wanaamini kuwa nyota huyo aliyepoteza umaarufu Old Trafford bado ana nafasi ya kuwa mchezaji tishio ndani ya muda mfupi ujao.
0 comments :
Post a Comment