Michezo ya Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 inaendelea kama kawaida kwa leo November 26 kwa michezo kadhaa kuchezwa, mechi kati ya Burnleydhidi ya Man City ilikuwa ni miongoni mwa michezo iliyochezwa leo.
Man City walikuwa ugenini katika dimba la Burnley kucheza mchezo wao huo wa 13 wa Ligi Kuu England, katika mchezo huo Man City walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, magoli ya Man City yakifungwa na Sergio Kun Aguerodakika ya 37 na 60 wakati goli la Burnley lilifungwa na Dean Marney dakika ya 14.
Kufuatia ushindi huo Sergio Aguero anakuwa kafanikiwa kuweka rekodi ya kuzifunga timu 29 kati 30 alizowahi kucheza nazo katika Ligi Kuu England.
1 - 2
Burnley
Manchester City
- D. Marney 14
- S. Agüero 37
- S. Agüero 60
Match Summary
Team line-up
0 comments :
Post a Comment