Habari zilizo-vuma sana leo kwenye upande wa soka ni kuanguka kwa ndege iliyokuwa imebeba wachezaji wa Chapecoense.
Sasa katika watu walionusurika katika ajali hiyo mbaya iliyotokea kwenye mji wa Medellin ni pamoja na beki wa pembeni Alan Ruschel.
Kwa mujibu wa ripoti, Ruschel alifika hospital akiwa macho huku akizungumza. Inatajwa kwamba alikuwa amevunjika sehemu kadhaa za mwili wake lakini alikuwa na majeraha kichwani pia.
Kwa mujibu wa waandishi wa Colombia, ameripoti kwamba, baada ya Ruschel kufikishwa hospital alikuwa na kitu kimoja tu akilini mwake ‘familia yake.’
Mchezaji huyo aliomba mtu amtunzie pete yake ya ndoa huku maswali yake yote hayakuwa juu ya afya yake bali ni kuhusu familia yake.
Mkewake aliposikia mumewe amenusurika kifo
Mke wa mchezaji huyo anayejulikana kwa jina la Alissen Rushel ali-post ujumbe kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupata taarifa kuwa mumewake amenusurika kutoka kwenye ajali hiyo ya ndege.
Kabla ya ndege haijaruka, Alan Ruschel alikuwa busy kwenye mitandao ya kijamii.
Alipost picha kadhaa kwenye ukurasa wake wa kijamii akionekana yupo ndani ya ndege.
0 comments :
Post a Comment