WENGER ATHIBITISHA KUA VERMAELEN ANAONDOKA!!
Yupo njiani? Beki wa ARSENAL, Thomas Vermaelen anaweza kujiunga na Barcelona. WAWAKILISHI wa Barcelona wapo mjini London kufanya mazungumzao ya kujaribu kumsajili Thomas Vermaelen kutoka ARSENAL ingawa wanakabiliana na Manchester United wanaohitaji saini ya beki huyo. Beki huyo mwenye miaka 28 amekuwa akihusishwa kuwindwa na klabu za Katalunya na United majira haya ya kiangazi, na Aserne Wenger ameshatibitisha kuwepo kwa dili hizo. Barcelona imemtuma mkurugenzi Raul Senlleh mjini London ili kufanya mazungumzo na ARSENAL
Vermaelen hakufanya mazoezi na ARSENAL siku ya jumanne kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya nyama za paja.
0 comments :
Post a Comment