Mtoto: Mourinho amesema hakutaka kumsajili Shaw kwasababu mshahara wake ni mkubwa sana.
JOSE Mourinho amesema
hakuthubutu kutaka kumsajili Luke Shaw kwasababu mshahara aliohitaji
kinda huyo `ungeua umoja’ wa timu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Shaw mwenye miaka 19, alisaini
Manchester United kwa dau la paundi milioni 30 na inasemekana atakuwa
analipwa mshahara wa paundi laki moja na elfu 20.
Mourinho alisema kiwango hicho ni kikubwa sana kwa klabu yake.
‘Kama
unamlipa mshahara mkubwa kijana mwenye miaka 19 Luke Shaw, tulikuwa
tunahitaji nini?, tungekufa’ alisema kocha wa Chelsea. “Tungeua umoja na
utulivu wetu katika matumizi ya hela. Tungeua umoja kwenye vyumba vya
kubadilishia nguo”.
“Kwasababu
unapomlipa zaidi mtoto wa miaka 19-mchezaji mzuri, wa ajabu-siku
inayofuata, mimi na (Mkurugenzi wa Chelsea) bwana Mrs Granovskaia na
(mkurugenzi wa ufundi) Michael Emenalo tutagongewa milango na wachezaji
wakisema inawezekanaje tumeichezea klabu mechi 200 na kushinda hili na
lile, lakini bwana mdogo anatuzidi mshahara?
“Inawezekanaje kijana wa miaka 19
anakuja hapa na kupata hela ambazo hata mimi sipati? ningeua usawa wa
timu na nisingeruhusu hilo kutokea”.
‘Filipe
Luis aliichezea Brazil, ameshinda makombe ya Ulaya, alicheza nusu
fainali ya UEFA, huyu mchezaji ni bei rahisi kuliko huyu mtoto wa
England?
“Sikosoi klabu nyingine kwa kumlipa vile. Lakini kwa klabu yangu, tunaweza kusema ingekuwa mbaya kwetu”.
0 comments :
Post a Comment