News
Loading...

Simba yaaga mashindano SportPesa

MWANA
Dar er Salaam.
 Mabingwa wa Kombe la FA, Simba imeaga mashindano ya Kombe la SportPesa kwa kufungwa kwa penalti 5 kwa 4 na Nakuru All Stars baada ya kumaliza dakika 90 kwa suluhu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Simba iliwatumia wachezaji wake wengi wapya ilitegeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini washambuliaji wake walikosa umakini katika umaliziaji.
Kuondolewa kwa Simba kunaifanya Yanga kuwa mwakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano hayo ya kusaka kucheza na Everton dhidi ya timu tatu za Kenya ambazo ni Gor Mahia, AFC Leopards na Nakuru zilizofuzu kwa nusu fainali.
Ndoto ya Simba kucheza nusu fainali ilipotea baada ya kipa Daniel Agyei kukosa penalti ya pili, ikiwa ni penalti pekee waliyopoteza.
Penalti za Simba zilifungwa na Besala Bokungu, Mwinyi Kazimoto, Hafidh Mussa na Finton Murenezo.
Kocha wa Nakuru, Maina George alisema timu yake ilipambana vikali na kufanikiwa kupata matokeo hayo.
Kagere aitupa nje Jang'ombe Boys
Mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Meddy Kagere yameiwezesha Gor
Mahia kufuzu nusu fainali ya mashindano ya Sports Pesa kwa kuifunga Jang'ombe Boys
mabao 2-0.
Kagere alifunga bao la kwanza dakika ya 64 kwa kichwa akimalizia krosi iliyopigwa na Innocent
Wahula.
Mshambuliaji huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akizitoa udenda klabu za Simba na
Yanga alifunga bao la pili dakika ya 83 kwa penalti baada ya mlinzi wa Jang'ombe kuunawa
mpira katika eneo la hatari.
Nusu fainali itachezwa Alhamisi kwa Yanga kuivaa AFC Leopards, wakati Gor Mahia itacheza dhidi ya Nakuru All Stars.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment