News
Loading...

MASHABIKI WA MAN UNITED MSIKILIZENI ERIC BAILLY ALIVYOWAJIBU REAL MADRID KUHUSU KUKIPIGA NAO MSIMU UJAO!!


MLINZI wa kati wa klabu ya Manchester United, Eric Bailly amewaambia Real Madrid kuachana na azma ya kutaka kumng’oa kwa sababu bado hana sababu ya kutaka kuachana na timu yake hiyo ya sasa, licha ya klabu hiyo ya Hispania kuvutiwa nae. Kwa msisitizo, Eric Bailly amesema anajisikia furaha ya maisha ndani ya klabu yake ya sasa kwenye viunga vya Old Trafford. Kauli ya Bailly inakuja siku chache baada ya kuwepo kwa uvumi kuwa vinara hao wa LaLiga wanataka kumng’oa Old Trafford kwa mapendekezo ya kocha Zinedine Zidane. “Taarifa hizi za klabu nyingi kunihitaji zinanipa faraja na heshima kubwa, lakini dhamira yangu ya sasa ni kuendelea kubaki hapa kwani bado nina kandarasi ndefu kuendelea kuwepo United,” alisisitiza. Kwa sasa beki huyo mwenye umri wa miaka 22 anatajwa kwenye dili la usajili Real Madrid. Madrid wametajwa katika mpango wa kuimarisha kikosi chao na Zinedine Zidane amesema bailly ni kati ya walinzi imara wa kuwajumuisha katika kikosi cha msimu ujao. Raia huyo wa Ivory Coast alithibitisha kusikia taarifa za kutakiwa na wakongwe hao, lakini akakanusha kuhusu kukubali kujiunga nao katika majira ya kiangazi.

 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment