News
Loading...

Sergio Aguero na Fernandinho watafungiwa FA wasema!!



Katika pambano liliopigwa jana kati ya Manchester City dhidi ya Chelsea katika dimba la Etihad Stadium wengi wetu tuliweza kushuhudia tukio la kibabe lililo fanywa na wachezaji wa klabu ya Manchester City katika dakika za mwisho wa mchezo huu.
Mechi iliyomalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Manchester City,magoli yaliyofungwa na Diego Costa,Willian na Eden Hazard huko goli la Manchester City lilipatikana kwa Gary Cahill kujifunga.
Sasa Shirikisho la Soka la England FA limetangaza kwamba litawafungia wachezaji wawili wa Man City kwa kile walicho kifanya katika mchezo huu maana si ungwana,Wachezaji ambao watahadhibiwa ni Mshambuliaji Sergio Aguero na kiungo Fernandinho.
Sergio Aguero aliweza kumchezea rafu mbaya sana beki wa Chelsea David Luiz na kumfanya kupata maumivu makali baada ya tukio hilo ndipo vurugu zikaibuka na mchezaji Fernandinho aliweza kuadhibiwa kwa kadi nyekundu baada ya kumkaba shingoni kiungo Cesc Fabregas kwa mkono wake pamoja na vidole.
Baada ya kuonyeshewa kadi nyekundu wachezaji hawa wawili na mwamuzi wa mchezo huo,FA imetoa tamko kwamba mchezaji Aguero huenda akafungiwa mechi 4 na Fernandinho mechi 3.
Aguero anakutana na kitanzi hiki kwa mara ya pili baada ya mwanzo wa ligi aliweza kupatiwa adhabu ya kufungiwa mechi tatu baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa West Ham United,Winston Reid.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment