LEO kuna kazi kubwa ndani ya Signal Iduna Park huko Jijini Dortmund Nchini Germany wakati Mafahali Wawili Borussia Dortmund na Bayern Munich watapokutana katika Mechi ya Bundesliga ambayo hubatizwa Jina la ‘Der Klassiker’.
Bayern ndio Mabingwa Watetezi wa Bundesliga na wapo Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 24 kwa Mechi 10 huku Dortmund wakiwa ni wa 5 wakiwa na Pointi 18 kwa Mechi 10.
Hivi sasa Bundesliga inaongozwa na Timu iliyopanda Daraja RB Leipzig ambao Jana walitwaa uongozi baada ya kutoka nyuma na kuibwaga Bayer Leverkusen 3-2.
Leipziga sasa wana Pointi 27 kwa Mechi 11.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Borussia Dortmund: Bürki - Piszczek, Papastathopoulos, Ginter, Guerreiro - Weigl - Dembelé, Castro, Götze, Schürrle - Aubameyang
Majeruhi: Bender, Durm, Subotic, Reus, Rode
Kocha: Thomas Tuchel
Bayern Munich: Neuer - Lahm, Boateng, Hummels, Alaba - Alonso - Thiago, Kimmich - Ribery, Müller – Lewandowski
Majeruhi: Coman, Robben, Martinez
Kocha: Carlo Ancelotti
BUNDESLIGA
Ratiba
Jumamosi Novemba 19
**Saa za Bongo
2030 Borussia Dortmund v Bayern Munich
1730 FSV Mainz 05 v Sport-Club Freiburg
1730 Borussia Monchengladbachv v FC Köln
1730 FC Augsburg v Hertha BSC
1730 SV Darmstadt 98 v FC Ingolstadt 04
1730 VfL Wolfsburg v FC Schalke 04
0 comments :
Post a Comment