Kwenu, Madridisno
Maisha yangu Real Madrid yamefikia mwisho. Ni ngumu kuandika yale yote
niliyopitia katika mistari michache, lakini nataka barua hii ifikishe
ujumbe wa kila ninachojisikia wakati huu wa kuagana. Katika hii miaka
minne nimepata heshima ya kuvaa jezi hii, hakuna ninachojisikia zaidi ya
kujivunia kwa kile nilichopitia na kufanikiwa pamoja na wenzangu.
SOMA ZAIDI HAPA
Bahati mbaya leo nalazimika kuondoka, lakini nataka kuweka hili wazi
haikuwa nia yangu. Kama mtu yeyote anayefanya kazi siku zote anataka
kusonga mbele. Baada ya kushinda ‘ La Decima’ nilienda katika kombe la
dunia nikiwa na matumaini ya kupata mkataba mpya ambao haukuja. Mambo
mengi na uongo mwingi ulizungumzwa. Siku zote walitaka kuanzisha kitu
ili mimi niondoke klabuni, lakini sikufanya hivyo.
Kitu pekee nilichoomba ni kile ambacho kingekuwa haki. Kuna vitu vingi
navithamini na vingi kati ya hivyo haviusiani kabisa na mshahara wangu.
Ninamatumaini nitasonga mbele. Manchester United ni moja ya klabu kubwa
duniani ambako ninataka kutengeneza historia. Nimekuwa na bahati sana ya
kutumia chumba kimoja cha kubadilishia nguo na wachezaji wazuri sana,
ambao wamekuwa marafiki wa kweli. Nadhani huo ndiyo ulikuwa ufunguo wa
La Decima.
Napenda kuomba radhi kutokana na kipindi nilichokosea uwanjani na nje ya
uwanja. Haikuwa nia yangu kuumiza mtu yeyote. Nilitoka jasho kwa ajili
ya jezi hii katika kila mechi nilidhani ilikuwa ni ya mwisho. Kulikuwa
na wakati mambo yalikuwa sawa kwangu kuliko kwa wengine, lakini
nachoweza kusema ni kuwa mara zote nilijitoa kwa uwezo wangu wote.
Nataka kuishukuru Hispania kwa kila kitu ilichonipa na hasa hasa
kuruhusu mwanangu kuzaliwa katika dunia hii. Na kwa watu muhimu sana wa
hospitali ya Monteprincipe, ambayo siku zote itakuwa moyoni mwangu. Mke
wangu, mwanangu na mimi siku zote tutaendelea kushukuru. Pia kwa
wachezaji wenzangu ambao walinipa sapoti siku zote kwenye wakati mzuri
na mbaya. Kwa watu wa ufundi nilifanya nao kazi na kwa wote wanaofanya
kazi siku klabuni ambao ninatumaini nitaendelea kuwa na uhusiano nao
mzuri daima.
Natumaini Real Madrid watakuwa na msimu mzuri sana na kupata mafanikio
ambayo klabu hii siku zote imekuwa ikiyatafuta. Siku zote nitakumbuka
muda ule kwenye Supercopa niliponyanyuka pale Bernabeu na nikapata
upendo wa kweli kutoka kwa mashabiki. Asanteni sana. Nilifurahi sana na
sikuwa na njia nyingine ya kuwaaga katika mechi ile ambayo bahati mbaya
ilikuwa mechi yangu ya mwisho.
Hala Madrid! Milele -
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment