News
Loading...

TFF YAJICHANGANYA SAKATA LA NGASSA, MENEJA TAIFA STARS AKILI WALIMUACHIA AENDE SAUZ

Hatimaye lile sakata la kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa kwenda kufanya majaribio nchini Afrika Kusini katika timu ya Free State Stars limepata majibu baada ya Meneja wa Taifa Stars, Boniface Clement, kusema kuwa wao ndiyo walimruhusu.

Awali kulizuka utata ambapo Yanga walitaka maelezo kuwa ni nani alimruhusu Ngassa kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Free State Stars bila ya ruhusa yao wakati wao walikuwa wanajua yuko kwenye kikosi cha Taifa Stars nchini Botswana.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa  likieleza kuwa hawahusiki na mchezaji huyo kwa kuwa hakuripoti katika kambi ya timu ya taifa alipoitwa.
Lakini Clement amesema kuwa, Ngassa aliomba ruhusa katika benchi la ufundi la timu hiyo ili aweze kwenda kufanya majaribio na kudai kuwa TFF hawakuwa wakijua.
“Ngassa hana tatizo kabisa na Stars na amejiunga na timu na anafanya mazoezi kama kawaida, kabla ya kuondoka alikuja kuomba ruhusa katika benchi la ufundi na aliruhusiwa.
“Kwa upande wa TFF hawakuwa wakijua suala hilo kwa kuwa wao ni watu wa ofisini, tutaendelea kuwa naye katika mechi dhidi ya Msumbiji kwani taarifa zake tulikuwanazo na hana shida,” alisema Clement.

Awali, Mwesigwa alisema Ngassa ameondolewa kwenye kikosi hicho kutokana na kocha kuchukizwa baada ya kuondoka bila ya kuaga.

Jana, Kocha Mart Nooij, akagoma kujibu swali hilo mbele ya waandishi wa habari na kuwataka wamfuate Ngassa hotelini na kumuuliza.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments :

Post a Comment